Na Samir Salum, Lango la habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itaendelea kuhakikisha haki za mtoto zinalindwa ikiwemo kuhakikisha wanapata ulinzi, huduma na elimu Bora.
Rais Samia ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Juni 16, 2022 ikiwa ni Maadhimisho ya Siku Mtoto wa Afrika yanayofanyika Juni 16 kila Mwaka yakiwa na lengo la kukumbuka mauaji ya kinyama waliyofanyiwa watoto wa kitongoji cha Soweto nchini Afrika ya Kusini mwaka 1976.
Rais Samia amewatakia kheri watoto na jamii nzima katika kuadhimisha Siku hii huku akiitaka jamii kutekeleza ajenda ya 2040 inayotaka Bara la Afrika kuwa sehemu bora ya watoto.
"Tuendelee kutekeleza Ajenda ya 2040 inayotaka Bara la Afrika kuwa sehemu bora kwa mtoto kwa kupata ulinzi na huduma bora, ikiwemo elimu" amesisitiza Rais Samia
Kitaifa maadhimisho ya Siku ya mtoto wa Afrika yanafanyika Jijini Dodoma yakiwa na kauli mbiu "Tuimarishe ulinzi wa mtoto, Tokomeza ukatili dhidi yake, tujiandae kuhesabiwa."
Mwisho