Na Lango La Habari
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi leo Ijumaa Juni 24, 2022 amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali.
Kupitia taarifa iliyotolewa leo Ijumaa Juni 24, 2022 Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi,Mussa Haji Ali imeeleza kuwa Rais Dkt. Mwinyi amemteua Khamis Ramadhan Abdallah kuwa Jaji Mkuu wa Zanzibar ambapo kabla ya Uteuzi huo Khamis alikuwa Anakaimu Wadhifa wa Jaji Mkuu wa Zanzibar.
Taarifa imeeleza kuwa Rais Mwinyi amewateua Majaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar ambao ni Salma Ali Hassan aliyekuwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), wapili ni Mohamed Ali Mohamed aliyekuwa Mrajis wa Mahakama Kuu ya Zanzibar.
Mwingine ni Said Hassan Said aliyekuwa Mwanasheria Mkuu katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Awamu ya Saba.
Aidha, Rais Mwinyi amemteua Salum Kassim Ali kuwa Mtakwimu Mkuu wa Serikali ambapo kabla ya Uteuzi huo Ndugu Salum alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Kusini Unguja.
Pia amemteua Dkt. Ali Salim Ali kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya UKIMWI Zanzibar. Dkt. Ali ni Mshauri wa Masuala ya Ukimwi katika Jumuiya ya ZAPHA.

Taarifa imeeleza kuwa Uteuzi huo unaanzia leo tarehe 24 Juni, 2022.