Breaking

Friday, 10 June 2022

PROFESA JAY ARUHUSIWA KUTOKA HOSPITALI



Hospitali ya Taifa Muhimbili imesema Joseph Haule (Profesa Jay) ameruhusiwa kutoka Hospitalini jana Alhamisi Juni 09, 2022 baada ya hali yake kiafya kuonekana kuimarika.




Msanii huyu nguli wa Bongofleva ameruhusiwa kutoka Hospitalini baada ya siku 127 za kutibiwa kwenye Hospitali hii ya Taifa iliyopo Jijini Dar es salaam.


Hata hivyo Familia yake imesema Nguli huyu hayupo nyumbani kwake bali sehemu yenye uangalizi maalum.

"Watu wanaweza kudhani kwakuwa Profesa Jay ametoka Hospitali wanaweza kudhani yupo tayari nyumbani, Mtu akiwa amekaa Hospitali kwa muda mrefu hauwezi moja kwa moja ukatoka ukaenda nyumbani bado kuna uangalizi anatakiwa aendelee kuupata, sio kwamba yupo nyumbani kwake ila ametoka Hospital ila yupo sehemu anapatiwa uangalizi maalum na sio nyumbani kwake" amesema Mdogo wake Black Rhyno
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages