Breaking

Thursday, 9 June 2022

PHIL FODEN ATWAA TUZO YA MCHEZAJI BORA CHIPUKIZI WA MWAKA


Na Ayoub Julius,Lango la habari 


Nyota wa Manchester City, Phil Foden ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi wa Mwaka wa PFA kwa msimu wa pili mfululizo, baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo hapo awali 2020/21. 


Foden alichangia pakubwa City iliposhinda taji la Ligi kuu Uingereza mbele ya Liverpool, tayari ni mara ya nne katika maisha yake akiwa na umri wa miaka 22 pekee. 


Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza alicheza mechi 28 za Premier League, akifunga mara tisa na kusaidia mabao matano. 


Katika mashindano yote, alimaliza akiwa na mabao 25 katika michezo 45. 


Pamoja na kuibuka kidedea katika Ligi kuu ya uingereza, City ya Foden ilifika nusu fainali ya Kombe la FA na Ligi ya Mabingwa. 


Foden tayari alikuwa ametawazwa kuwa Mchezaji Chipukizi wa Ligi Kuu ya Uingereza kwa Msimu wa 2021/22, tuzo nyingine kuu ambayo alikuwa ameshinda hapo awali 2020/21. 


Ni wachezaji wachache tu katika historia ya tuzo za PFA ndio wamechaguliwa kuwa Mchezaji Bora Chipukizi wa Mwaka katika msimu uliofuata. 


Wa mwisho kufanya hivyo alikuwa Dele Alli mnamo 2017, huku Foden akijiunga na kundi la washindi mfululizo ambao ni pamoja na Wayne Rooney, Robbie Fowler na Ryan Giggs.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages