Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa amekutana na kuzungumza na Meneja wa Kampuni ya Noble Helium Joseph Uisso inayofanya utafiti wa gesi ya Helium katika maeneo ya Bonde la Ziwa Rukwa, Eyasi, Nyasa na Manyara.
Dkt. Kiruswa amekutana nao leo Juni 2022, katika kikao kifupi kilichofanyika katika ukumbi wa wizara Jijini Dodoma.
Katika kikao hicho, Dkt. Kiruswa na uongozi wa Kampuni ya Noble Helium wamezungumzia kuhusu maendeleo ya shughuli za utafiti zinazoendelea katika maeneo hayo.
Aidha ameahidi kushughulikia changamoto zote walizonazo mapema.