Breaking

Tuesday, 21 June 2022

MWANAFUNZI WA DARASA LA SABA AUAWA NA KUTUPWA PEMBENI YA MTO - GEITA



Jeshi la polisi Mkoa wa Geita linachunguza kifo cha aliyekuwa mwanafunzi wa Darasa la Saba, Johson Thomas (14) katika shule ya msingi ya Buhalahala Halmashauri ya Mji ya Geita mkoani Geita aliyekutwa amefariki na mwili wake ukiwa pembeni mwa mto baada ya kupotea Juni,12 2022

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo june 21,2022 Kamanda wa Jeshi la polisi Kamishina Msaidizi, Henry Mwibambe amesema Mwili wa marehemu ( Johnson ) ulikutwa una majeraha kwenye mguu wa kushoto na mguu mwingine umepondwa na kitu kizito kwenye unyayo.

Kamanda Mwaibambe amesema uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa mtoto huyo alitoka nyumbani kwao kwa kutumia usafiri wa bajaji iliyokuwa inaendeshwa na Benson Theophili June,12 ,2022 Majira ya saa kumi na Moja jioni kuelekea buhalala Center kupeleka sare za shule kwa ajili ya kushonewa.

"Tunachunguza ili tujue chanzo cha Mauaji ya mtoto kwa sababu mara ya mwisho alipakizwa kwenye bajaji ya Familia iliyokuwa inaendeshwa na huyo Benson na alimtelemshia njiani Bila kumfikisha Center Sasa kwanin alimwacha Njiani?". alihoji Mwaibambe

"Utata ni mkubwa kwenye hiki Kifo chake kwa sababu hata fundi alipokuwa anakwenda ni kwa fundi wa familia au mtoto alikuwa anaenda kwa fundi Yoyote ?". Alisema Mwaibambe

Aidha mwaibambe ameomba Wazazi na walezi kutoa taarifa mapema katika jeshi la polisi pindi mtoto anapokuwa hajaonekana masaa 24 sio mpaka zipite siku Mbili ,tatu ndo wanatoa taarifa .


Source: Wasafi Media
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages