Breaking

Thursday, 2 June 2022

MWANAFUNZI WA DARASA LA PILI ABAKWA NA KUAWA KWA CHANDARUA




POLISI mkoani Pwani wanamsaka mtu mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa mwenye umri kati ya miaka 30 na 40 kwa tuhuma za kumnajisi na kumua kwa kumziba na chandarua mdomoni, mwanafunzi wa darasa la pili shule ya Msingi Misugusugu mwenye umri wa miaka Saba (7).


Kijana huyo anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka (40) alimfanyia kitendo hicho cha unyama mwanafunzi huyo wa darasa la pili Shule ya Msingi Misugusugu.


Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, ACP Pius Lutumo imesema kuwa, mtuhumiwa alitendea tukio hilo nyumbani kwake.


Amesema kuwa, tukio hilo limetokea Mei 30,mwaka huu huko mtaa wa Vitendo Misugusugu Kata ya Misugusugu wilayani Kibaha ambapo baada ya tukio hilo mtuhumiwa huyo alitoroka.


Lutumo amesema kuwa, uchunguzi wa awali umebaini kuwa mtuhumiwa alifanya tukio hilo la mauaji wakati akimbaka mwanafunzi huyo ambapo aliziba mdomo kwa kutumia chandarua ili asipige kelele na kusapabisha kifo hicho.


Aidha, ametoa wito kwa wazazi na walezi kwa kueleza kuwa wanapaswa kuwafuatilia watoto wao na kuzungumza nao mara kwa mara juu ya kujilinda wenyewe ka kutoa taarifa za haraka juu ya wanaowasumbua.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages