Mwanamke mmoja anayefahamika kwa jina la Maria Matheo, anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Tabora kwa tuhuma za kumuua mume wake, Gabriel Nguwa (80) kwa kumkaba shingoni akiwa amelala.
Akithibitisha tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora ACP Richard Abwao amesema kuwa tukio hilo limetokea Mei 30 mwaka huu majira ya saa nane usiku katika kitongoji cha Bugwed, Kijiji cha Budushi, Kata ya Budushi wilayani Nzega mkoani Tabora.
Kamanda abwayo amesema kuwa Maria ilimvizia mume wake akiwa amelala na kumkaba shingoni na kumsababishia kifo.
Ameelezea chanzo cha mauaji hayo kuwa wanandoa hao walikua na mgogoro wa muda mrefu.
"nyakati za jioni ambapo mke anapolewa huwa anamtuhumu mumewe kuwa hakuwa na msaada wowote katika maisha yao" Ameelezea Kamanda Abwao
Amesema mtuhumiwa amekamatwa na upelelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani kwa ajili ya taratibu za kisheria.
Amesema mtuhumiwa amekamatwa na upelelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani kwa ajili ya taratibu za kisheria.