OJADACT inalaani matukio ya mauaji yanayoendelea Nchini husasani matukio mawili ya mauaji ya watoto yaliyotokea Mkoani Geita, tukio la kwanza lilihusisha kifo cha aliyekuwa Mwanafunzi wa Darasa la saba Johson Thomas (14) katika shule ya Msingi Buhalahala , Halmashauri ya Mji Geita, Mkoa wa Geita, aliyekutwa amefariki na mwili wake ukiwa pembeni mwa Mto baada ya kupotea Juni 2, 2022.
Tukio la pili ni tukio la kuuawa kwa mtoto Dorcas Mathias mwenye umri wa Miaka (7) aliyekuwa Mwanafunzi wa Chekechea Shule ya Msingi Ibambi Wilaya ya Nyahg’wale Mkoani Geita baada ya kuvamiwa na watu watatu wakati akiwa aanachunga mbuzi na mwenzake.
Kamanda wa Polisi Mkoani Geita Henry Mwaibambe alisema baada ya mwili huo kufanyiwa uchunguzi na Daktari alibainika kuwa,Dorcas alibakwa, kulawitiwa na kisha kuuawa na baadaye akavunjwa shingo. Jeshi la Polisi limewafikisha Mahakamani watuhumiwa watatu Mathias Shilole (52),Mganga wa tiba asili na Mkazi waKilimanajro Nyangwale na LucyMdelema kwa tuhuma za kujihususha na mauaji hayo.
OJADACT imebaini sababu mbalimbali za maujai hayo ni pamoja na
1.Imani za kishirikina kwenye jamii zinahusishwa na kujipatia utajiri kwa njia nyepesi
2.Ukatili kwenye jamii unaombatana na malezi mabaya ya jamii isiyo na staha
OJADACT inatoa rai kwa jamii kutojihusisha na vitendo vya uvunjifu wa sheria na badala yake jamii iwe mlinzi wa mtoto kwa kutoa tarifa inapoona viashiria vya ukiukwaji wa haki za mtoto ikiwemo haki ya kuishi .
Serikali na wadau mbalimbali wanendelee kufanya kazi kwa pamoja ya kumlinda mtoto.
Edwin Soko
Mwenyekiti
OJADACT
22.06.2022