Na Lango La Habari
Majambazi watatu wameuawa baada ya kupambana na Jeshi la Polisi wakiwa katika harakati za kutaka kupora katika duka, eneo la Goba Dar es Salaam.
Akithibitisha tukio Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam Jumanne Murilo amesema kuwa tukio hilo limetokea leo Ijumaa Juni 24, 2022 majira ya saa 6:45 mchana eneo la Goba Tegeta A, Wilaya ya Ubungo kwenye duka la miamala ya kifedha lililopo eneo lililofahamika kama Skymart Mini supermarket.
Amesema kundi la majambazi wanne wakiwa na pikipiki namba MC 469 CMT aina ya TVS wakiwa wamejihami kwa silaha za moto, walifika eneo hilo kwa lengo la kuvamia na kupora fedha katika duka hilo.
Kamanda Muliro Amesema taarifa zilitolewa haraka na askari Polisi walipofika eneo hilo walianza kushambuliwa kwa risasi na katika mazingira hayo askari namba F3625 SGT Eliamini alijeruhiwa kwa risasi chini ya bega karibu na kifua.
Majambazi nao walishambuliwa na kujeruhiwa vibaya, ambapo walipelekwa haraka hospitali lakini kwa bahati mbaya watatu wamepoteza maisha na mmoja alitoroka. Hali ya askari aliyejeruhiwa inaendelea vizuri
Uchunguzi wa awali (Criminal Record) umeonesha kuwa kati ya majambazi hao, wawili wametambuliwa kuwa ni Ridhiwani Sunna Mgeni @Babu Ally aliyewahi kushtakiwa kwa kesi ya Mauaji PI 148/2006 na Rajabu Ramadhani @Rogers aliyewahi kushtakiwa kwa mauaji PI 28/2014.
Majambazi hao wamekutwa na silaha mbili aina ya Long rifle 22 iliyotengenezwa Ubelgiji yenye Risasi 11 pamoja na Pistol aina ya Star yenye Risasi 6.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam linaendelea na ufuatiliaji wa makundi yote yanayojihusisha na kupanga njama, na kujaribu kutelekeza vitendo vya kihalifu, kuwa halitavumilia na halitasita kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria