Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kinondoni imetupilia mbali na kuiondoa kesi iliyokuwa ikimkabili aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda juu ya matumizi mabaya ya Ofisi na kuingilia matangazo ya kielektroniki ktk kituo cha TV na Radio cha Clouds Media.
Uamuzi huo umetolewa leo na Hakimu Mfawidhi Aron Lyamuya ambapo amesema Mahakama hiyo haina Mamlaka ya kusikiliza shauri hilo kwa kuwa makosa yaliyotajwa hayaipi Mahakama hiyo uwezo wa kuyashughulikia.
Kutokana na hatua hiyo, Makonda hana kesi inayomkabili katika mahakama hiyo, hii imetokana na Mbunge wa zamani wa Ubungo Kubenea kupitia Mawakili wake kumshitaki Makonda katika kesi ya jinai namba 7, 2021.
Miongoni mwa tuhuma alizodai Kubenea ni matumizi mabaya ya madaraka huku Watuhumiwa wengine wakiwa ni Mkurugenzi wa Mashitaka na DCI.