Breaking

Monday, 27 June 2022

CHADEMA WAWEKA PINGAMIZI KESI YA KINA MDEE, MAHAKAMA YATOA ZUIO UBUNGE WAO




Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, leo Jumatatu Juni 27, 2022 imetoa zuio la muda kuhusu kutofanyika chochote kwenye Ubunge wa Halima Mdee na wenzake 18 mpaka pale Mahakama hiyo itakaposikiliza maombi ya Rufaa yao.

Hatua hiyo imekuja baada ya 
CHADEMA kupitia kwa mawakili wake akiwemo Peter Kibatala, kuwasilisha pingamizi la awali wakipinga maombi mapya ya akina Mdee dhidi yao ambapo wanaiomba mahakama hiyo iwape kibali cha kufungua kesi ya kupinga kuvuliwa uanachama wa chama hicho. 

Mdee na wenzake wamefungua maombi Mahakama Kuu dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa Chadema (iliyosajiliwa) wakiomba ridhaa ya kufungua shauri la kupinga kuvuliwa uanachama wa Chadema.

Sambamba na maombi hayo ya ridhaa namba 27 ya mwaka 2022, pia wamefungua maombi ya amri ya zuio dhidi ya NEC na Spika, kutochukua hatua dhidi ya uamuzi wa Chadema kuwavua uanachama.

Maombi hayo yaliyopangwa kusikilizwa na Jaji Mustapha Ismail yametajwa leo Jumatatu Juni 27,2022, ndipo mawakili wa Chadema wakaibua pingamizi, dhidi ya maombi hayo ya zuio.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages