Breaking

Wednesday, 22 June 2022

MAHAKAMA YATUPILIA MBALI KESI YA MDEE NA WENZAKE 18



Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Kuu ya Dar es Salaam imetupilia mbali kesi ya msingi iliyokuwa imefunguliwa na wabunge 19 waliovuliwa uanachama na CHADEMA iliyokuwa ikipinga kuvuliwa uanachama wao na Baraza Kuu la CHAMA hicho hivyo kuruhusu taratibu zingine kuendelea.

Chadema Iliwafukuza rasmi wabunge hao Mei 12, 2022, kwenye mkutano wao mkuu uliofanyika Mlimani City ambapo baada ya hapo walifungua kesi ya pingamizi katika mahakama kuu ambayo ndiyo imetolewa maamuzi leo.

Wabunge hao 19 wa Chadema waliingia bungeni baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, ambapo Chadema ilijitokeza hadharani mara kadhaa kukanusha kuwa sio wabunge Wao.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages