Wizara ya Afya imetoa taarifa kuhusu mwenendo wa Covid-19 katika kipindi cha tarehe 05 Mei hadi 03 Juni 2022 ambapo maambukizi mapya 161 yamethibitika ikilinganishwa na maambukizi 68 kwa kipindi cha tarehe 02 Aprili hadi 4 Mei 2022.
Dar es Salaam imeripoti visa 130, Arusha (10), Mwanza (5), Shinyanga (4), Mtwara (3), Dodoma (2), Mara (2), Morogoro, (1), Simiyu (1), Katavi (1), Kilimanjaro (1) na Mbeya (1)