Na Vintan Godfrid
Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya ubeligiji na Klabu ya Chelsea Romelu Lukaku amefanikisha nia yake kurudi katika ligi kuu ya Nchini italia katika klabu ya Inter Milan.
Klabu ya Chelsea na Inter Milan wamefikia makubaliano ya kumrudisha mshambuliaji huyo katika ligi kuu ya italia kwa mkopo wa ada ya Euro milioni 8 (€8 milioni) na maongezo kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Lukaku aliuzwa kutoka Inter kuelekea klabu ya Chelsea katika ligi ya uingereza msimu wa mwaka 2021/2022 ambapo hakuweza kufanikisha kile mashabiki wengi wa Chelsea walicho kitarajia.
Lukaku alikuwa na wakati bora sana katika ligi kuu ya italia ambapo alifunga jumla ya magoli 64 katika mechi 95, kwa misimu aliocheza ndani ya klabu hiyo.
Kwa upande wa Chelsea lukaku toka arejee alifunga magoli 15 katika mechi 44 alizocheza klabuni hapo kitu ambacho hakikuweza kuridhisha mashabiki wengi wa Chelsea ukizingatia na ada ya uhamisho Euro milioni 97.5 (£ 97.5 milion) kutoka Inter Milan.
Lukaku alikuwa mara kadhaa akionyesha wazi wazi nia ya kutaka kurudi Inter na hatimae matamanio take yamezaa matunda kwa mkopo wa mwaka mmoja kuitumikia tena miamba hiyo kutoka nchini Italia.