Breaking

Friday, 10 June 2022

LIVERPOOL WATAMBA KIKOSI CHA MWAKA UINGEREZA PFA 2021/2022

Na Ayoub Julius,Lango la habari 


Manchester City wanaweza kuwa wameipiku Liverpool taji la Ligi kuu Uingereza lakini Majogoo hao ndio wanaatawala Kikosi Bora cha Ligi Kuu ya Uingereza PFA 2021/22. 


Wachezaji sita wa Liverpool wametajwa kwenye kikosi hicho, kilichopigiwa kura na wachezaji wenzao wa Premier League, akiwemo kipa Alisson Becker na mabeki Trent Alexander-Arnold na Virgil van Dijk. 


Kiungo machachari Thiago Alcantara pia anatajwa kwenye kikosi kutokana na uchezaji wake katika safu ya kiungo, huku haishangazi kuona washambuliaji wawili mahiri Mohamed Salah na Sadio Mane wakitajwa mbele. 


Salah, kwa bahati pia aliteuliwa kuwa Mchezaji Bora wa Mwaka wa Wachezaji wa PFA kwa 2022. 

Joao Cancelo, Kevin De Bruyne na Bernardo Silva ni wachezaji watatu wa Manchester City wanaounda timu, na pia kuna nafasi kwa Antonio Rudiger katika safu ya ulinzi. 


Mjerumani huyo ataondoka Chelsea hivi karibuni kwenda kwa washindi wa Ligi ya Mabingwa, Real Madrid. 


Cristiano Ronaldo, licha ya msimu mbaya wa Manchester United, pia anatajwa kuwa mbele baada ya kupachika mabao 18 ya Ligi Kuu ya Uingereza katika msimu wake wa kwanza kurejea England. 


Kikosi Bora cha Ligi Kuu ya PFA - 2021/2022


• GK: Alisson Becker (Liverpool) 


• DF: Trent Alexander-Arnold (Liverpool) 


• DF: Virgil van Dijk (Liverpool) 


• DF: Antonio Rudiger (Chelsea) 


• DF: Joao Cancelo (Manchester City) 


• MF: Kevin De Bruyne (Manchester City) 


• MF: Thiago Alcantara (Liverpool) 


• MF: Bernardo Silva (Manchester City) 


• FW: Mohamed Salah (Liverpool) 


• FW: Cristiano Ronaldo (Manchester United) 


• FW: Sadio Mane (Liverpool)

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages