Na Said Muhibu, Lango La Habari
Uwanja wa Benjamin Mkapa uliopo jijini Dar es salaam Tanzania umechaguliwa kuwa miongoni mwa viwanja vitakavyotumika kwenye michuano ya raundi ya kwanza na ya pili ya michezo ya kufuzu fainali za Mataifa bingwa Afrika (CHAN) itakayoanza kutimua vumbi mnamo Julai 22, 2022.
Taarifa iliyotolewa na shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) imesema uwanja wa Mkapa ni miongoni mwa viwanja vitatu vya Kanda ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) vilivyopitishwa kutumika kwenye michuano ya kufuzu fainali CHAN.
Viwanja vyengine vya kanda ya CECAFA ambavyo navyo vimethibitishwa kuchezeshewa michuano hiyo ni pamoja na St Mary's, Uganda na Al Hilal, Sudan.
Aidha, michezo ya raundi ya kwanza itachezwa kati ya Julai 22-24, 2022 na marudiano itakuwa kati ya Julai 29-31, 2022.
Kwa upande mwengine Tanzania itakabiliana na Somalia kwenye raundi ya kwanza ya mashindano hayo ambayo yanahusisha wachezaji wa ndani.
Kombe la Mataifa ya Afrika (CHAN) ni shindano kuu la la soka la kimataifa barani Afrika na husimamiwa na shirikisho la mpira wa miguu Afrika (CAF). ililichezwa kwa mara ya kwanza mwaka wa 1957 na tangu mwaka wa 1968 shindano hili limekuwa likifanyika kila baada ya miaka miwili.