Breaking

Tuesday, 14 June 2022

KOCHA TIMU YA TAIFA YA UINGEREZA ATOA ONYO KWA RASHFORD, SANCHO



Na Vintan Haulle

Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Uingereza Gareth South ameweka bayana kuwa wachezaji wawili wa Manchester United, Jadon Sancho na Marcus Rashford wanahitaji kazi ya ziada ikiwa wanataka kuingia kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza .


Wachezaji hao wote hawako kwenye mpango wa kocha msimu huu wa majira ya joto katika mashindano ya Uefa Cup of Nations kutokana na timu yao kufanya vibaya msimu wa 2021/2022 yanayoendelea ikiwa ni hatua ya makundi sasa.


Harry Maguire ni mchezaji pekee wa Manchester United ambae amefanikiwa kuingia kwenye kikosi cha Simba watatu.

South amekuwa mkweli na mwenye matumaini juu ya wachezaji hao ila wakati huu amekuwa mkali kwa kutoa onyo kwa wachezaji hao wa mashetani wekundu


 Amesema  anatoa nafasi kwa kila mchezaji anaeonyesha kiwango na utayari kwa maana kuna aina ya wachezaji ambao huwa wako tayari muda wowote kucheza na wale wengine ambao huwa wanahitaji muda kupumzika kila baada ya mechi.


Nafasi bado zipo za kufanya mabadiliko katika kikosi kuelekea kombe la dunia 2022 huko Qatar kwa hivyo wachezaji watakao onyesha kiwango katika timu zao watajumuishwa katika Kikosi cha Simba watatu.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages