Na Ayoub Julius,Lango la habari
Mchezo wa Kufuzu AFCON 2023 katika hatua za makundi umetamatika kwa bao 2-0 katika uwanja wa Taifa kwa Mkapa Jiji Dar es Salaam ambapo Taifa Stars alikuwa nyumbani dhidi ya Mashujaa wa Jangwani Algeria.
Bao la kwanza Algeria likifungwa na Ramy Bensebaini dakika ya 47' ya mchezo kipindi cha kwanza na msumari wa mwisho ukikomelewa na Mohamed Amoura mnamo dakika ya 89' ya mchezo.
Tangu mwaka 2015 Tanzania na Algeria wamecheza michezo mitano na Algeria amefanikiwa kutamba mara 4 na kutoa sare mara moja pekee.
Kipigo kikubwa ni kile cha tarehe 17 Mwezi Novemba Mwaka 2015 ambapo Tanzania ilikubali kichapo cha bao 7-0 ikishuhudiwa Mudathiri Yahya kuonyeshwa kadi nyekundu mnamo dakika 41' ya mchezo.
Katika msimamo wa kundi F Algeria anashika nafasi ya kwanza akiwa na alama 6 akifuatiwa na Niger mwenye alama 2 ,Tanzania ikisha nafasi ya tatu kwa alama 1 na mwisho ni Uganda the Craine wakiwa na alama 1 pekee ikiwa ni tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa kati yake na Tanzania.