Breaking

Friday, 17 June 2022

DEREVA BAJAJI AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA JELA KWA KUMBAKA MTOTO WA MIAKA 10




Mahakama ya Wilaya ya Iringa imemhukumu kifungo cha maisha na fidia ya shilingi milioni 7 dereva wa Bajaji, John Umbo (20) baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumbaka mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 10.

Mahakama imetoa hukumu hiyo jana Alhamisi Juni 16, 2022 baada ya kujiridhisha na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka.

Katika kesi hiyo, Umbo alidaiwa kufanya kitemdo hicho Mei Mosi, 2022 baada ya kumrubuni mtoto huyo anayesoma moja ya shule za msingi za mjini Iringa na kumpeleka vichakani kisha kumtisha kwa kumwambia achague kuuawa au kubakwa.

Akitoa hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mkuu Saidi Ally Mkasiwa amesema kuwa mahakama imetoa hukumu baada ya kumkuta na tuhuma hizo licha ya kumpa nafasi mtuhumiwa kujitetea lakini alibaki kimya hivyo.

Imeelezwa kuwa Mtuhumiwa huyo amewahi kuwa na kesi kadhaa za ukatili wa kijinsia siku za nyuma na alifikishwa Mahakamani lakini hakuwahi kukutwa na hatia.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages