Breaking

Saturday, 11 June 2022

DC SHIMO ATAKA UTUNZAJI VYANZO VYA MAJI WILAYA YA GEITA


Mkuu wa wilaya ya Geita, Wilson Shimo amezitaka jumuiya za watoa huduma za maji  ngazi ya Jamii  (CBWSO’s) kuongeza weledi katika utunzaji wa vyanzo vya maji ili viweze kuwa endelevu na salama kwa watumiaji.


Mhe Shimo amesema hayo katika mkutano mkuu wa vyombo vya watoa huduma ya maji ngazi ya jamii (CBWSO’s) wilayani Geita  kilichofanyika katika ukumbi wa alphendo amesema jumuiya hizo zinapaswa kutunza vyanzo vya maji katika maeneo yao.


Amesema  swala la kutunza vyanzo vya maji ni jukumu la kila mmoja  hasa jumuiya za watoa huduma za maji ngazi ya jamii ili kutoa maji safi na salama kwa wananchi.

Amewata kupanda miti ambayo ni rafiki na maji katika  vyanzo vya maji ili kuweza kuvitunza pamoja na kulinda vyanzo hivyo ili wananchi wa maeneo husika waweze kupata maji safi na salama.


Hata hivyo  Shimo ameipongeza   Ruwasa wilaya ya Geita kwa kuendelea kusimamia na kutekeleza  vyema miradi mbalimbali ya maji ndani ya halmashauri ya wilaya ya Geita.

Kwa upande wake Meneja wa Ruwasa Wilaya ya Geita Sande Batakanwa amemuhakikishia Mhe, Wilson Shimo kuwa atahikisha anasimamia vyema Jumuiya za watoa huduma ya maji ngazi ya jamii (CBWSO) ili ziweze kusimamia vyema vyanzo vya maji.


Sande amesema  atasimamia kikamilifu zoezi la upandaji miti rafiki katika vyanzo vya maji kama alivyoagiza mhe, mkuu wa wilaya kwa lengo la kuhakikisha vyanzo vya maji vinalindwa pamoja na kutunzwa ili viweze kutoa maji kwa mda mrefu.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages