Mtoto Erickson Kimaro mwenye umri wa miaka nane amedaiwa kuuawa kwa kunyongwa na msichana wa kazi nyumbani kwao Kimara Temboni Dar es Salaam.
Inadaiwa Mfanyakazi huyo wa ndani alifika kwenye nyumba hiyo ya mwajiri wake siku ya Jumamosi 28 Mei, 2022. Ameshinda siku ya Jumapili nyumbani na Jumatatu Mtoto alivyorudi kutoka shule mfanyakazi huyo akamnyonga mpaka kufariki dunia.
Inadaiwa waajiri wa huyo binti walikuwa bado hawajamfahamu Vizuri binti huyo kwasababu ya kuwa busy tokea afike kwenye nyumba yao. Mama ni Daktari wa Moyo Hospitali ya Temeke, huku Baba akiwa ni Daktari wa Wanawake Hospitali ya Mloganzila.
Inadaiwa binti baada ya kumuua mtoto huyo, alimpigia simu mama mtoto mida saa 11:30 jioni na kumweleza kuwa mtoto anaumwa na anashindwa kupumua vizuri. Baada ya Mama kufika akakuta mtoto ashakuwa wa baridi kichwani ila kiwiliwili cha moto, baada ya mtoto kukimbizwa Hospitali ya Mloganzila ilithibitika ameshafariki dunia.
Shahidi anazidi kuelezea kuwa Binti wa kazi alichukuliwa na Jeshi la Polisi na bahati nzuri nyumba ilikuwa imefungwa Kamera za ulinzi na walipoangalia waliona kuwa Binti wa kazi ndiye aliyehusika na mauaji hayo kwa kumnyonga mtoto huyo asiye na hatia.