Ayoub Julius,Lango la habari
Cardiff City wako tayari kutoa ofa za kandarasi kwa magwiji wa Wales Gareth Bale na Aaron Ramsey.
Bale aliisaidia nchi yake kupata nafasi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia la 2022 siku ya Jumapili, kwa mpira wa faulo uliishia wavuni mwa Ukraine kutokana na mpira mbaya uliopigwa na Andriy Yarmolenko, ambapo alitania kwamba mipango yake ya kustaafu ilikuwa imesitishwa kwa muda.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 sasa analenga kutafuta klabu mpya kwa ajili ya msimu wa 2022/23 na vyanzo vimethibitisha kwamba Cardiff wako tayari kumtumia Bale kwa ujasiri.
Bale hajawahi kucheza soka la klabu huko Wales lakini alizaliwa Cardiff na Bluebirds wanatumai kutumia ukaribu wake kuelekea kuitumikia nchi yake ili kumnasa kwa mkataba wa muda mfupi ambao wanatumai unaweza kurefushwa zaidi ya kampeni zijazo ikiwa Cardiff itarejea 'Premier League' Ingawa mishahara inayotolewa kwenye michuano hiyo haiko karibu na pauni 600,000 kwa wiki ambayo Bale aliichukua akiwa Real, anafahamika kuwa yuko tayari kukatwa mshahara mkubwa ili kujiunga na klabu yake ijayo.
Pamoja na Bale, Cardiff wako tayari kutupa kofia yao ulingoni kwa Ramsey, nyota mwingine wa Wales ambaye anaweza kuhama msimu huu wa joto.
Uhamisho wa Ramsey, ambaye aliingia katika akademi ya Cardiff, unatatizwa na ukweli kwamba bado ana miezi 12 kwenye mkataba wake na Juventus, lakini timu hiyo ya Serie A inatarajiwa kufanya kila wawezalo kuachana na Ramsey msimu huu wa joto na inaweza kumfanya apatikane kwa uhamisho wa bure.