Breaking

Wednesday, 15 June 2022

BREAKING: WATU WATANO WAFARIKI DUNIA, WATANO WAJERUHIWA AJALI YA BASI SHINYANGA


Na Samir Salum, Lango la habari


Watu watano wamefariki dunia na wengine watano wakijeruhiwa baada ya Basi la Zuberi linalofanya safari za Mwanza - Kahama kugonga kingo za daraja na kupinduka katika eneo la Mwigumbi Mkoani Shinyanga.

 

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando amesema kuwa ajali hiyo imetokea leo Jumatano Juni 15, 2022 majira ya saa nane mchana katika barabara ya Mwanza Shinyanga ambapo basi hilo lenye namba za usajili T435 DJS SCANIA liligonga ukingo wa daraja la Mwigumbi na kutumbukia bondeni.


Kamanda Kyando amesema waliofariki ni Wanawake Wawili, Wanaume wawili na Mtoto mmoja huku kati yao ni dereva wa basi hilo aliyefahamika kwa jina la Hamza Haule.


Amesema chanzo cha ajali hiyo ni dereva alipata tatizo la kiafya akiwa safarini.


Aidha, ametoa wito kwa madereva kuchunguza afya zao kabla ya kuanza safari ili kuepusha ajali zisizo za lazima.





Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages