Breaking

Friday, 10 June 2022

AJALI YAUA WATU 19 NA KUJERUHI 8 IRINGA





Watu 19 wamefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa katika ajali iliyotokea eneo la Mafinga mkiani Iringa leo Ijumaa Juni 10, 2022.


Ajali hiyo imehusisha Lori aina ya Scania lenye namba za usajili T 736 AAE lililokuwa limebeba mchanga na Coaster yenye namba za usajili T 542 DQV.

Akithibitisha kutokea ajali hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, ACP Allan Bukumbi amesema ajali imesababisha vifo zaidi ya 10 akisema kuwa taarifa ziaidi zitatolewa baadaye

"Ni kweli ajali imetokea na inasadikika watu zaidi 10 wamepoteza maisha papo hapo," amesema.

Akitoa taarifa kwa Mkurugenzi wa Mji wa Mafinga, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Mafinga, Dk. Victor Msafiri amesema ajali hiyo imesababisha vifo vya watu 19 na majeruhi ambao bado wanaendelea kupatiwa matibabu.

Amesema majeruhi wanaendelea kupata matibabu na miilii ya marehemu baadhi imeshatambulika na wengine wanaendelea kutambuliwa na jeshi la polisi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mafinga Mji, Happiness Laizer amewatembelea majeruhi na kuwapa pole huku akiwaomba Madaktari kuwapa hudumu stahiki ili hali zao ziweze kutengemaa kwa haraka.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages