Breaking

Tuesday, 7 June 2022

ATAFUTWA KWA KUMUUA MKE WAKE KWA KUMCHOMA NA KITU CHENYE NCHA KALI



Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamtafuta Mwanaume mmoja ambaye ni mkazi wa Mazizini Ukonga kwa tuhuma za kumuua mke wake, Logesara Chitemo kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali.

Kamanda wa Polisi Kanda hiyo, Jumanne Muliro amesema tukio hilo lilitokea Juni 6, 2022 ambapo marehemu alikuwa anauza pombe ya kienyeji ndipo walianza ugomvi ambapo mume wake.

Amesema kuwa baada ya kuibuka ugomvi kati ya wawili hao, mume alimchoma mkewe na kitu chenye ncha kali na kumsababishia majeraha kifuani na kichwani na baadaye kufariki dunia.

Kamanda Muliro amesema mtuhumiwa huyo baada ya kufanya kitendo hicho alikimbia kusikojulikana.

"Jeshi la Polisi linaendelea kumtafuta mtuhumiwa huyo na lazima tutampata na tutamfikisha kwenye vyombo vya sheria,"amesema Muliro.

Ametoa rai kwa wananchi pale inapotokea migogoro kwenye familia kushirikisha ndugu au taasisi za kidini na vyombo vya kisheria kikiwamo ya ustawi wa jamii pamoja na mahakama ili kutatua migogoro hiyo.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages