Breaking

Saturday, 4 June 2022

ASKARI WAWILI MBARONI KWA KUUA MTUHUMIWA KWA KUMPIGA RISASI - MOROGORO




Jeshi la polisi Mkoani Morogoro linawashikilia askari wawili kwa mahojiano zaidi kwa tuhuma za kumuua kwa kumpiga kumpiga risasi Hamiss Hassan (30) mkazi wa mvuha wilayani Morogoro

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa polisi Mkoa wa Morogoro Fortunatus Muslim amesema tukio hiko lilitokea Mei 30, 2022 ambapo askari no_ G8808 D/CPL Mapalala na no_ G8626D/CPL Patrice wote kutoka kituo cha mvua walitumwa na mkuu wa kituo hicho kwenda kumkamata Hamiss Hassan.

Kamanda Muslim ameeleza kuwa Hamis alikuwa anatuhumiwa kufyeka shamba la ufuta baada ya kutofautiana na mwenza wake ambaye alienda kumshitaki katika kituo cha polisi Mvua.

Amesema kuwa mara baada ya kufika alilokuwa mtuhumiwa askari Mapalala akiwa amebeba silaha aina ya AK-47 yenye no_ 5002573 alianza kumkimbiza mtuhumiwa na baadaye aliamuwa kumpiga risasi chini ya goti ili kumdhibiti asiendelee kukimbia.

Mtuhumiwa alifariki dunia baada ya kuvuja damu nyingi akiwa anapatiwa matibabu katika hospital ya wilaya.


Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages