Breaking

Saturday, 18 June 2022

ASAKWA KWA KUMUUA MKE WAKE KWA KUMLIMA NA JEMBE KICHWANI








JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamsaka fundi wa majokofu, Godbles Sawe (47), anayetuhumiwa kumuua mke wake Ester Gadau.

Akithibitisha tukio hilo Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Jumanne Muliro, amesema kuwa mauaji hayo yametokea Jumanne Juni 14, 2022 eneo la Kibamba wilayani Ubungo.

Kamanda Muliro mesema kuwa Sawe ambaye ni mkazi wa Kimara Suka mkoani Dar es Salaam, anatuhumiwa kumuua mke wake, Ester Gadau, kwa kumkata kichwani kwa kutumia kitu chenye ncha kali na kumsababishia umauti kisha kukimbia baada ya mauaji hayo.

Akisimulia tukio hilo Diwani wa Kibamba, Peter Kilango amesema kuwa mtuhumiwa alifanya tukio hilo majira ya saa 12.30 jioni kwa kumlima na jembe kichwa kisha kukimbilia kusikojulikana kwa kutumia usafiri wa bodaboda.

Diwani Kilango amesema mtuhumiwa huyo ambaye ni Mchaga wa Machame anajishughulisha na kazi ya kutengeneza friji ambapo siku ya tukio mtuhumiwa alitoka nyumbani na kumuacha mkewe akikanda unga wa ngano kwa ajili ya kuchoma maandazi.

“Mke wake ni mjasiriamali anafanya kazi ya kuchoma maandani na vitumbua na wakati anatengeneza vitu vyake kwa ajili ya kuchoma maandazi na vitumbua, alitoka na kwenda kununua mkaa,” alisema Kilango.

Aliongeza kuwa baada ya Ester kurudi alikuta mlango umefungwa na kushangaa kuwa nani amefunga, mwanamke huyo aliwauliza majirani na kujibiwa kuwa mume wake ambapo alivyogundua ni mume wake aliamua kwenda kwa mjumbe kwa kuwa hawakuwa na uhusiano mzuri na mumewe.

Alieleza kuwa baada ya mjumbe kuelezwa, alikuja na kugonga mlango na mtuhimwa akafungua na kumuamuru mkewe aingine ndani lakini mkewe akakataa kuingia. Aliongeza kuwa kwa kuwa majirani wanafahamu ugomvi wao waliondoka wakiamini kuwa wataelewana tu.

“Wakati wakiwa nje ya nyumba yao mtuhumiwa akamwita mtoto wao anaitwa Ben anasoma darasa la saba Kibamba, lakini mke akamjibu kuwa Ben hayupo nimemtuma dukani. Jibu hilo lilimkasirisha yule bwana wakati amsehikilia jembe anajifanya analima ghafla akamkimbiza mkewe na kumpiga na jembe kichwani,” aliongeza Kilango.

Baada ya mkewe kuanguka chini mtuhumiwa alianza kumponda kichwa mithili ya kulima hali iliyosababisha kupasua kichwa na kukiharibu kabisa. Wananchi waliposhtuka na kujaribu kumkata alikimbia na kufika barabarani na kupanda bodaboda na kutokomea kusikojulikana.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages