KATIKA hali ya kusikitisha Mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina la Bunanzi Kulwa maarufu kama Ngosha Mkazi wa Mbagala kwa mbiku jijini Dar es salaam anadaiwa kumuua mpenzi wake aliyefahamika kwa jina la Happines Zakarika kisha nae kujiua kwa kunywa sumu, huku chanzo kikiwa bado hakijajulikana.
Tukio liho limetokea Juni 8 mwaka huu, huku likizua sintofahamu kwa majirani wa eneo hilo kutokana na marehemu hao kuishi kama dada na kaka kwa takribani miaka 2.
Waandishi wa Global Publisher Issa mnaly na Richard Bukos wamefika eneo la tukio na kuzungumza kwa kina na Rafiki wa karibu wa Marehemu Ngosha aliyejitambulisha kwa jina la Shineneko Ruge ambaye anabainisha kuwa marehemu alikuwa ni rafiki yake wa karibu.
Ruge amesema kuwa usiku mmoja kabla ya kifo cha marehemu alimpigia simu mama yake mzazi na kumuambia kuwa atajitoa uhai.
Aidha Ruge amebainisha kuwa siku moja kabla ya kufariki alikuwa na rafiki yake huyo ambaye kwa sasa ni marehemu na moja kati ya maongezi yao ni kwamba alimuaga kuwa atasafiri yeye na dada yake kwenda Marekani hivyo alikuwa akifuatilia masuala ya Visa, lakini Ruge anasikitika kwa kusema kuwa hakufahamu kama hiyo ndiyo ilikuwa safari yake ya mwisho hapa duniani.
Source: Global Publisher