Watu watano wamekufa papo hapo na wengine tisa wamejeruhiwa baada ya basi dogo aina Coaster waliyokuwa wamepanda kuacha njia na kupinduka.
Mkuu wa Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga, Kalisti Lazaro amesema ajali hiyo imetokea jana Ijumaa Juni katika Kijiji cha Mbaramo Tarafa ya Umba wilayani humo.
Lazaro amesema gari hilo lilikuwa lenarejea Dar es Salaam kutoka Kijiji cha Mbaramo kupeleka msiba.
Mkuu huyo wa wilaya ametaja majina ya waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni Sebastian Kamwedi (35), Msambaa Godfrey Martin (70), Jackline Shemela (37), Emanuel Philipo mtoto wa miezi miwili na Elly Gumbo.
Amesema majeruhi sita wamepelekwa katika Hospital ya Rufaa Bombo mkoani Tanga huku watatu wakiwa wanaendelea kupata matibabu katika Kituo cha Afya Mnazi kilichopo wilayni Lushoto.
Inadaiwa kuwa dereva wa gari hilo alishindwa kulimudu kwenye kona hali iliyosababisha gari hilo kupinduka.
Lazaro ametoa wito kwa madereva wageni wanapopanda milima ya Usambara wawe makini.
Source: Mwananchi