Breaking

Monday, 6 June 2022

AJALI YA BASI YAUA WATU 22 HUKU SABA WAKIJERUHIWA - INDIA




Takriban watu 22 wamefariki dunia, wengine saba kujeruhiwa vibaya huku mmoja akiwa hajulikani alipo baada ya basi moja kutumbukia kwenye korongo eneo la milimani kaskazini mwa India.

Akizungumza na Shirika la Habari la AFP msimamizi wa polisi wa Wilaya ya Uttarakhand, Arpan Yaduvanshi amesema kuwa ajali hiyo imetokea jana Jumapili Juni 05, 2022 majira ya jioni ambapo Basi hilo lililokuwa limebeba watu 30 akiwemo dereva lilikuwa linaelekea Yamunotri, eneo la mbali la Hija la Wahindu katika jimbo la Himalaya la Uttarakhand.

Imeelezwa kuwa ajali hiyo ilitokea Uttarkashi, takriban kilomita 160 kutoka mji mkuu wa jimbo la Dehradun ambapo Polisi wamethitisha vifo 22.

"Watu waliojeruhiwa wamekimbizwa katika vituo vya matibabu vilivyo karibu," msimamizi wa polisi wa wilaya Arpan Yaduvanshi aliiambia AFP.

Yaduvanshi aliongeza kuwa wafanyikazi wa uokoaji bado walikuwa wakitafuta abiria aliyepotea na idadi ya vifo "inaweza kuongezeka zaidi".

Waziri wa Mambo ya Ndani wa India Amit Shah alisema kwamba alikuwa akiwasiliana na viongozi wa eneo hilo kuhusu kazi inayoendelea ya kutoa misaada kwa tukio hilo "la kusikitisha sana".

Kwa mujibu wa Serikali ya India, inakadiriwa watu 150,000 hufariki dunia kila mwaka kutokana na ajali huku sababu kubwa zikitajwa kuwa mwendokasi na wananchi kutofunga mikanda na kuvaa kofia ngumu

Miongoni mwa sababu kuu zinazochangia vifo vingi ni mwendokasi kupita kiasi na watu kutofunga mikanda au kuvaa helmeti za ajali.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages