Breaking

Wednesday, 8 June 2022

AHUKUMIWA MIAKA 30 JELA KWA KUMBAKA MAMA YAKE MZAZI - IRINGA



Na Mwandishi Wetu, Iringa

Mahakama ya Wilaya ya Iringa imemuhukumu kifungo cha mika 30 na fidia ya Tsh. Milioni 1 Mfanyabiashara Kaloli Mkusa (30) mkazi wa kijiji cha Msisina kwa kosa la kumbaka Mama yake Mzazi.

Hata hivyo Mtuhumiwa na Baba yake Joseph Mkusa ambaye alimuwekea dhamana wametoweka kusikojulikana na hati ya kukamatwa tayari imetolewa.

Akitoa Hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama hiyo Emmy Msangalufu amesema Mtuhumiwa alifanya tukio hilo May 07,2021 ambapo siku ya tukio Mtuhumiwa alikwenda nyumbani kwa Mama yake majira ya usiku na kuvunja mlango huku akiwa ameshika panga na kumtisha kumkata kwa kumpiga na ubapa wa upanga.

Licha ya Mama yake kumsihi asifanye hivyo lakini Mtuhumiwa aliendelea na kumbaka Mama yake mpaka alipomaliza, baada ya tukio Mama alitoa taarifa kwa majirani baadae Serikali ya Kijiji ndipo taratibu za kumkamata zikafanyika.

Tukio Hilo linasadikiwa ni kutokana na Imani za kushirikiana kutokana na biashara ya Mtuhumiwa kuyumba, Mtuhumiwa alikuwa akifanya biashara zake Tunduma Mkoani Songwe na alirudi akafikia kwa Baba yake ambaye anaishi nyumba tofauti na Mama yake kutokana na kupeana talaka.

Hata hivyo hati ya kukamatwa ilitolewa Tareh 09/03/2022 lakini mpaka Sasa Mtuhumiwa pamoja na Baba yake aliyemuwekea dhamani hawajulikani walipo, kwa mujibu wa Mahakama kifungo hicho kitaanza kutumika pindi Mtuhumiwa atakapokamatwa.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages