Mahakama ya Wilaya ya Iringa imemuhukumu kifungo cha maisha na fidia ya Tsh. Million 10 Mkulima Ramadhan Musa Chewa (34) Mkazi wa Pawaga kwa kosa la kumuingilia kinyume na maumbile Mtoto wa kike wa Dada yake mwenye umri wa miaka 12 aliyekuwa akisoma darasa la nne katika Shule ya Msingi M-boliboli.
Akitoa Hukumu hiyo katika Mahakama ya Wilaya Hakimu Mkazi Mkuu Said Ally Mkasiwa amesema Mtuhumiwa alitenda kosa hilo April 04,2020.
Mtuhumiwa alikwenda kusalimia kwa Dada yake na akawa analala sebuleni na ilipofika siku ya tatu Dada yake alikwenda kuchota maji asubuhi ndipo Mtuhumiwa akaingia chumbani alipokuwa amelala Mtoto huyo na kumlawiti.
Mwendesha Mashtaka wa Serikali Nashon Saimon aliiomba Mahakama kutoa adhabu Kali kutokana na Mtoto kufanyiwa kitendo kisicho na maadili Cha kuingiliwa kinyume na maumbile lakini pia kitendo hicho kimemuathiri kisaikolojia na kimaumbile na adhabu iwe fundisho kwa Mtuhumiwa na wote wenye tabia Kama hizo.
Aidha Mahakama ilipompa nafasi ya kujitetea Mtuhumiwa Ramadhan Musa Chewa aliomba apewe msamaha wa Kifungo na upande wa fidia alisema ana dhamba lake heka moja lipo Eneo la Pawaga na atamfidia Muathirika hata hivyo Mahakama ikamkuta na hatia na imempa kifungo cha maisha na fidia ya Milioni 10.