Breaking

Thursday, 9 June 2022

ACHOMWA KISU SHINGONI KISA KUDAI ELFU MOJA - NJOMBE




Mtu mmoja anayejulikana kwa jina la Mbaraka Madege Muuzaji wa nyama ya kuchoma katika mtaa wa Kibedange Halmashauri ya Mji wa Makambako Mkoani Njombe amechomwa na kisu shingoni kwa kosa la kumdai shilingi elfu moja Mteja wake.

Akizungumza kwa shida huku akiuguza jeraha lake Madege amesema amechomwa na kisu na Mteja wake Oswadi Kihombo aliyekuwa amefika katika eneo lake la kuuzia nyama mara baada ya kukataliwa kupewa nyama baada ya kukopa kutokana na kudaiwa kiasi cha shilingi elfu moja ya nyama ya awali.

"Alifika kwangu akakopa nyama nikamkatalia kwa kuwa ninamdai elfu moja nyingine, akanivamia tukio lilikuwa ndio hilo ila kwa sasa naendelea vizuri japo shingo inanisumbua" Madege

Rajabu Shayo ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Kibedange amethibitisha kutokea kwa tukio hilo katika Mtaa wake na kufafanua kuwa alifika Hospitali na kukuta kijana huyo akiendelea kupata matibabu huku Mtuhumiwa akiwa tayari ameshikiliwa na Polisi Kituo cha Makambako.


"Kwakweli kama Mtu anatembea na silaha ina maana huyu Mtu ni mbaya angemkosa huyu ina maana angemchoma hata Mtu mwingine ila niwaambie tu Wananchi kuwa dawa ya deni ni kulipa"



Source: Millard Ayo
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages