Mwanaume mmoja kutoka Pakistani aliefahamika kwa jina la Yahya almaarufu Pappu ameripotiwa kuchoma moto kaburi la Mama Mkwe wake aliyefariki miaka 25 iliyopita huko Layyah, jimbo la Punjab.
Mwanaume huyo alilimwagia petroli kaburi hilo na kutishia kutuma picha za eneo hilo kwa Mke wake wa zamani, suala hilo lilikuja baada ya Mke wake wa zamani ambaye walipeana talaka miaka 10 iliyopita kutaka kuolewa tena, jambo ambalo alikataa.
Shemeji yake ambaye amefungua kesi amesema Mwanaume huyo alichoma kaburi hilo baada ya kukasirishwa na kukataliwa na Mke wake wa zamani
“Kwakuwa Dada yangu amemkataa na amepata taarifa za kuolewa kwake ameamua kuchoma kaburi la Mama yetu”
Msemaji wa polisi amesema kaburi hilo limepatikana likiwa na dalili za kuchomwa moto, na Mtu huyo amekamatwa na atafikishwa Mahakamani.