Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. George Simbachawene (kushoto) akizungumza na Balozi wa Algeria nchini, Mhe.Ahmed Djellal alipomtembelea ofisini kwake Bungeni Mei 31, 2022 Jijini Dodoma.Balozi wa Algeria nchini, Mhe. Ahmed Djellal akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili ofisini kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. George Simbachawene Bungeni Mei 31, 2022 Jijini Dodoma.Mkurugenzi Idara ya Bunge na Siasa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Raymond Kaseko (kushoto) na Mchumi Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. William Babu wakifuatilia mazungumzo wakati wa kikao hicho.Balozi wa Algeria nchini, Mhe.Ahmed Djellal akieleza jambo alipokutana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. George Simbachawene ofisini kwake Bungeni Mei 31, 2022 Jijini Dodoma.Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. George Simbachawene akisalimiana na Balozi wa Algeria nchini Tanzania, Mhe. Ahmed Djellal alipomtembelea ofisini kwake Bungeni Mei 31, 2022 Jijini Dodoma.
************
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Algeria nchini Tanzania Mhe. Ahmed Djellal alipomtembelea ofisini kwake Bungeni Mei 31, 2022 Jijini Dodoma.
Katika mazungumzo hayo masuala mbalimbali yalijadiliwa ikiwemo kudumisha ushirikiano bana ya Tanzania na Algeria katika kuhakikisha ustawi wa Nchi zote mbili pamoja na raia wake.
Balozi wa Algeria alipongeza jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuweka mazingira rafiki ya biashara na uwekezaji nchini huku akiahidi kutoa ushirikiano katika kuimarisha mahusiano yaliyopo.
MWISHO