Breaking

Monday, 2 May 2022

WAZIRI NAPE AWATAKA WANAHABARI AFRIKA KUSAIDIA JUHUDI ZA MAENDELEO




Waziri wa Habari, Mawasiliano na Technolojia ya habari, Nnape Nnauye amewataka waandishi wa habari barani Afrika, kusaidia maendeleo ya bara hilo lenye rasilimali nyingi lakini wananchi wake ni masikini.

Akizungumza leo Mei 2 katika warsha ya maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari Duniani (WPFD) jijini Arusha, Nnape amewataka wanahabari kubadilisha hali hiyo.

"Nadhani umefika wakati wanahabari kusimama kusaidia kubadilisha mambo hayo na inawezekana Kila Mmoja akiamua kutimiza wajibu wake," amesema Nape.

Nnape amesema wanahabari wanapojadili maendeleo ya sayansi na Technolojia ni muhimu kuona namna ambayo sekta ya habari inasaidia jamii kuziona fursa za mabadiliko ya technolojia.

Amesema hivi sasa haiwekani kuendelea kusubiri wakati wakati watu wengine wanakimbia.


"Leo hapa nchini kuna mjadala juu ya mifumo ya kulipa kielekroni Kuna wengine wanahofu lakini ni wajibu wa vyombo vya habari kusaidia kufanya chambuzi juu ya jambo hili," amesema.

Amesema ni vizuri vyombo vya habari kuendelea kulindaja kuendelea uhuru, ramilimali na utamaduni wa Afrika na maslahi ya Afrika.

Waandishi wa habari na wadau wa habari zaidi ya 300 wanashiriki katika Warsha kuelekea maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari Duniani (WPFD).



Source: Mwananchi 
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages