Breaking

Friday, 20 May 2022

WAZIRI MCHENGERWA MGENI RASMI MISS TANZANIA USIKU HUU MEI 20, 2022




Na John Mapepele

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa usiku wa leo Mei, 20, 2022 ndiye Mgeni Rasmi kwenye kilele cha kumpata Miss Tanzania wa mwaka huu.

Shindano hili linafanyika jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Mlima City huku likipambwa na burudani kali kutoka kwa vikundi mbalimbali vya burudani.



Wadau mbalimbali urembo na mitindo wamefurika kujionea mrembo mmoja kati ya warembo washiriki 20 atakayeipeperusha bendera ya Tanzania kwenye mashindano ya dunia.




Pamoja na zawadi nyingine mshindi wa kwanza ataondoka na gari dogo aina ya benzi lenye thamani ya milioni thelathini na kitita cha shilingi milioni kumi, mshindi wa pili milioni tano huku mshindi wa tatu akiondoka na milioni tatu.







Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages