Breaking

Tuesday, 3 May 2022

WAZIRI MCHENGERWA, DKT. ABBASI WASHIRIKI SWALA YA EID EL FITRI, MUFTI ASISITIZA ZOEZI LA SENSA







Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa na Katibu Mkuu wa Wizara yake, Dkt. Hassan Abbasi leo Mei 3, 2022 wameungana na Viongozi Wakuu wa Nchi na waumini wa dini ya Kiislamu kushiriki Swala ya Eid El Fitri iliyofanyika kitaifa katika Msikiti Mkuu wa BAKWATA Kinondoni Muslim Jijini Dar es Salaam.




Swala hiyo imeongozwa na Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zubeir na kuhudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu. Mhe, Kassim Majaliwa Majaliwa.



Katika Swala hiyo, Mufti wa Tanzania ametoa wito kwa waislam wote nchini kujitokeza na kushiriki kikamifu zoezi la kitaifa la Sensa litakalofanyika Agosti 23 mwaka huu nchini.


Mufti Zubeir amefafanua kwamba muislam kukataa kuhesabiwa kwa kigezo kuwa kitendo cha kuhesabiwa ni haramu siyo msingi wa dini ya kiislam na kuwataka kushiriki kikamilifu zoezi hilo kwa maendeleo ya taifa letu kwa ujumla.



"Sensa ipo na Serikali imetuwekea utaratibu mzuri na sisi viongozi wa Dini tuwe mstari wa mbele kuhamasisha waumini wetu kushiriki kwenye sensa ili watanzania wote tuhesabiwe na kufanikisha lengo la kujua idadi halisi ya Wananchi na makazi"- ameongeza MUFTI.

Ameongeza kuwa sensa ni zoezi muhimu kwa taifa lolote duniani kwa kuwa linasaidia Serikali kupanga mipango mbalimbali ya maendeleo kwa ufanisi.




Aidha MUFTI Zuber amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutengeneza filamu ya Royal Tour na kusema filamu hiyo imeitangaza Tanzania ulimwenguni na kuvutia watalii kuja kutembelea vivutio hapa nchini na hivyo Taifa kuingiza Pato na kuzalisha Ajira huku akiwataka watanzania kujivunia filamu hiyo na kuendelea kuitangaza kwa juhudi zote.






Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages