Breaking

Friday, 27 May 2022

WAZIRI MCHENGERWA ATOA NENO SIKU YA UTAMADUNI WA VYAKULA ASILI VYA UTURUKI


Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa amesema kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na Uturuki kwenye sekta za Utamaduni na Sanaa kwa faida ya nchi zote mbili.


Waziri Mchengerwa ametoa kauli hiyo jana   leo Mei 26, 2022  katika kilele cha siku ya Utamaduni wa vyakula vya asili vya Uturuki kwenye ubalozi wa Uturuki jijini Dar es Salaam ambapo wasanii mbalimbali wa filamu na muziki walihudhuria.

Licha ya kuishukuru Serikali ya Uturuki kwa kujenga kituo cha utamaduni hapa nchini Waziri Mchengerwa amesema Tanzania itaendeleza  ushirikiano huo kwenye sekta ya Utamaduni ikiwa ni pamoja na kubadilishana uzoefu katika eneo la wataalam wa Utamaduni.


Amesema kuwa Mwaka huu Tanzania inakwenda kuadhimisha siku ya kiswahili duniani kuanzia Julai mosi hadi kilele chake Julai saba  kwa kufanya program mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufanya maonesho ya mapishi ya vyakula vya asili kutoka kwenye mbalimbali nchini. 

Ameiarika Uturuki  kushiriki kwenye maadhimisho ya siku hiyo kwa kuonesha vyakula  asili vya nchi hiyo kama ambavyo mataifa mbalimbali yatakavyoshiriki huku akiipongeza Uturuki kwa kuendelea kutangaza lugha ya kiswahili duniani kupitia filamu zao zinazotafsiriwa kwa lugha ya kiswahili.


Kwa upande wake Balozi wa Uturuki nchini. Mhe, Dkt. Mehmet Gulluoglu amesema ameishukuru Serikali ya Tanzania na kuahidi ushirikiano kwenye sekta za Utamaduni na Sanaa kwa faida ya nchi zote mbili.

Hafla hiyo imepambwa na msanii Godfrey Kapandila ambaye alitoa burudani ya nyimbo kadhaa ikiwemo malaika.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages