Breaking

Monday, 23 May 2022

WAZIRI BASHUNGWA AONYA HALMASHAURI ZINAZOTOA MIKOPO KWA VIKUNDI HEWA, ATOA MAAGIZO KWA MA-DED


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Innocent Bashungwa ametoa onyo kwa halmashauri kutoa mikopo kwenye vikundi hewa na kwa watu ambao sio walengwa wa mikopo hiyo.


Pia ameagiza wakurugenzi wa majiji, manispaa na miji ambayo inakusanya mapato zaidi ya Shilingi bilioni 5, kutenga na kutoa fedha asilimia 10 kwa ajili ya kuimarisha barabara za mitaa.


Bashungwa ameyasema hayo jijini hapa wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya mfumo wa usimamizi wa mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ya halmashauri kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.


Amesema baada ya kukamilika kwa mafunzo hayo hataki kusikia vikundi hewa au fedha za mikopo zinakwenda Kwa wasiowalengwa.


" Baada ya mafunzo haya, masuala ya vikundi hewa lazima yajadiliwe na tutoke na mkakati wa kuyadhibiti, ili iwe ni historia tusisikie mambo ya vikundi hewa. 


" Pia watu wasiolengwa na fedha hizi, lazima mfumo huu na kikao kazi hiki kiangalie baada ya mafunzo haya hatutaki kusikia watu wasiolengwa wanapata mikopo"


Bashungwa alisisitiza kuwa waliopewa mafunzo hayo wahakikishe wanafuatilia mikopo iliyotolewa kwa vikundi ili kuwe na tija na mkopo ubadikishe maisha ya wanufaika.


 " Sitakimkuona mikopo inatolewa ili mradi unatiki kwamba imetoa, tunataka tija kwenye mikopo hii, hivyo mnaopewa mafunzo hakikisheni mnafutalia mikopo hiyo ili kuhakikisha inayokwenda kusaidia kubadilisha maisha yao, suala la tija ni muhimu sana."


Bashungwa pia amesisitiza kuhakikisha urejeshaji wa mikopo hiyo inakuwa wa hali ya juu ili fedha hizo zitumike na vikundi vingine.


"Kwanza nishukuru kwa kuja na mfumo huu na ni njia sahihi ya kutekeleza maelekezo ya CAG kwenye maeneo ambayo tumeelekezwa upande wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI hususani ni kwenye fedha za asilimia 10 na usimamizi wake limekuwa ni hoja inayojirudia kwa CAG lakini na Bunge kupitia Kamati za LAAC na USEMI limekuwa likitoa maoni na mapendekezo kila mwaka ni hayo hayo."


Sasa Changamoto hizi zimefika mwisho niwataka Mamlaka zote za Serikali za Mitaa kuhakikisha wanatumia vyema mfumo huu katika utoaji wa mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages