Breaking

Wednesday, 11 May 2022

WAWILI MBARONI KWA KUBAKA NA KUUA MTWARA




Jeshi la polisi Mkoani Mtwara, linawashikilia watu wawili na mmoja bado anatafutwa na jeshi hilo kwa tuhuma za kumbaka kisha kumuua Elizabet Steven Peter (41) mkazi wa Kijiji cha Mkajamila wilaya ya Masasi Mkoani humo.

Akithibitisha tukio hilo  Kaimu Kamanda Jeshi la Polisi mkoani humo, ACP Nicodemus Katembo amesema Mei 6, 2022 Jeshi la Polisi lilipokea taarifa ya kukutwa mwili wa Elizabeth katika mtaa wa Mkunguni Wilayani Masasi.

Katembo amesema watuhumiwa hao walimbaka marehemu na kisha kumvunja shingo kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

"Polisi walianza upelelezi kupitia Wataalamu wa Cyber na kumkamata Innocent Ndomba (32) ambaye alikiri kuhusika na tukio kwa kushirikiana na Mume wa Marehemu Deograthias John (32) ambaye anashikiliwa pia na Polisi" ameelezea

"Watuhumiwa wameleeza kuwa chanzo cha tukio ni wivu wa kimapenzi baina ya Marehemu na Mumewe ambapo inadaiwa Marehemu alikuwa akimroga Mumewe pamoja na kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Wanaume wengine" Ameongeza ACP Katembo


Aidha katika tukio lingine Polisi mkoani Mtwara wanafanya uchunguzi wa kifo cha Hassan Mumwela, (35) mfanyabiashara na mkazi wa Kijiji cha Namhi Kata ya Libobe Wilaya ya Mtwara, baada ya mfanyabiashara huyo, kuanguka ghafla na kupoteza maisha akiwa katika eneo lake la biashara
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages