Breaking

Tuesday, 10 May 2022

WATOTO WATUHUMIWA KUKODI MUUAJI WA MAMA YAO MZAZI TABORA





Jeshi la Polisi mkoani Tabora limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa wa mauaji ya mwanamke aliyefahamika kwa jina la Nyanzobe Bukangala mkazi wa Kijiji cha Chamwabo wilayani Nzega.

Kwa mujibu wa Polisi, chanzo cha mauaji hayo ni imani za kishirikana ambapo inadaiwa kuwa mtuhumiwa huyo alikodiwa na watoto wa marehemu ili atekeleze mauaji hayo kwa madai kwa kulipa kisasi baada ya kumshutumu mama yao huyo alimroga Baba yao mzazi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, ACP Richard Abwao amesema tukio hilo lilitokea Mei saba (7) ambapo mtuhumiwa huyo anadaiwa alimkatakata mapanga mwanamke huyo na uchunguzi bado unaendelea huku mtuhumiwa akiwa mikononi mwa Jeshi hilo.


Aidha katika hatua nyingine Jeshi la Polisi mkoani Tabora likiwa katika Kampeni ya kukabiliana na matukio ya mauaji limefanikiwa kuwatia nguvuni watuhumiwa watatu wa tukio la mauaji ya kumchinja Maimuna Bakari Matuzya mkazi wa Kijiji cha Usupilo wilayani Sikonge ambaye anadaiwa kuuawa saa tano usiku mwishoni mwa mwezi Aprili na kisha mwili wake kutelekezwa kwenye shamba la jirani, Kata ya Misheni wilayani Sikonge huku chanzo cha tukio kikitajwa kuwa ni imani za kishirikina.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages