Watu wasiojulikana wameteketeza gari la Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Nyamilanda, Wilaya ya Muleba mkoani Kagera, Emmanuel Jonathan.
Gari hilo aina ya Toyota Harrier limeteketezwa usiku wa Jumapili Mei 08, 2022 wakati hakimu huyo akiwa amelala nyumbani kwake.
Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Toba Nguvila ameagiza Jeshi la Polisi wilayani humo kufanya uchunguzi ili kuwabaini watu waliofanya kitendo hicho.
Nguvila ametoa agizo hilo mara baada ya kutembelea eneo la tukio Jumatatu Mei 09, 2022 na kisha kuzungumza na wananchi
"Ninaagiza Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi na kuwabaini watu waliofanya tukio hilo ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria kutokana na kujichukulia sheria mkononi," amesema Nguvila.
Kwa upande wake Hakimu huyo amesema kuwa, siku ya tukio akiwa amelala usiku aliamshwa na vijana wa kazi kuwa gari linaungua moto ndipo aliamka na kuanza kuzima moto kwa kushirikiana na majirani ingawa gari lilikuwa limeshateketea.