Mke na mume wakazi wa Mtaa wa Lwenge, Halmashauri ya Mji Geita, wamenusurika kifo baada ya kutuhumiwa kuiba nyanya Shambani.
Wanandoa hao ambao ni Hamis Hassan na Mkewe Ester Edward wanatuhumiwa kufanya uhalifu huo wa wizi wa mazao mnamo Mei 17 na Mei 18, 2022 ambapo walikamatwa.
Akizungumza kwenye ofisi ya serikali za mtaa huo baada ya kukamatwa kijana huyo aitwa amesema ni kweli alikuwa shambani na mkewe lakini kasingiziwa kwa kitendo cha wizi huku Mke wake amesema hajui kama mme wake ana jihusisha na vitendo hivyo huku akisema alichukuliwa na Mme wake akamwambia amfate ndipo walipofika shambani na kukutwa na tuhuma hiyo.
Kwa upande wao wamiliki wa shamba hilo wanasema njia waliyotumia kuhakikisha wanamkamata mtu aliyeiba mazao yao.
Naye Mtendaji wa Kata ya Kalangalala Hamad Hussein, amekiri kutokea kwa tukio la kukamatwa kwa wanandoa hao kwa tuhuma za wizi huku akiwataka wananchi kujiepusha kujichukulia sheria za nchi.
Naye Mtendaji wa Kata ya Kalangalala Hamad Hussein, amekiri kutokea kwa tukio la kukamatwa kwa wanandoa hao kwa tuhuma za wizi huku akiwataka wananchi kujiepusha kujichukulia sheria za nchi.
Source: EATV