Na Said Muhibu,Lango la habari
Ofisa wa shirika la afya ulimwenguni WHO na mtaalamu wa magonjwa ya kuambukiza David Heymann amesema kuwa ugonjwa wa homa ya nyani unaenea kwa kasi sana ulimwenguni kama magonjwa ya zinaa.
kauli hiyo ameitoa hii leo Mei 22, 2022 kutokana na ugonjwa huo kuenezwa kwa mgusano wa karibu na hivyo kuwapata watu wengi ulimwenguni tangu kuripotiwa kwa ugonjwa huo.
"Kinachoonekana kutokea sasa ni kwamba imeingia katika idadi ya watu kama njia ya ngono, katika mfumo wa uzazi, na inaenezwa kama magonjwa ya zinaa, ambayo yameongeza maambukizi yake duniani kote," David Heymann alisema.
Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa lilisema, kufikia Jumamosi, kesi 92 zilizothibitishwa na kesi 28 zinazoshukiwa za ugonjwa wa homa ya nyani, ziliripotiwa kutoka nchi 12 ikiwemo; Uingereza, Hispania na Marekani. Shirika hilo liliongeza kuwa, litatoa mwongozo na mapendekezo zaidi katika siku zijazo kwa nchi mbalimbali juu ya kukabiliana na ugonjwa huo.
Homa ya nyani ni ugonjwa wa kuambukiza ambao unapatikana sehemu za Afrika Magharibi na Kati.
Ingawa ni ya familia ya virusi sawa na ndui, dalili zake ni kali zaidi. Kwa kawaida watu hupona ndani ya wiki mbili hadi nne bila kuhitaji kulazwa hospitalini, lakini maradhi hayo huwa hatari.