Breaking

Wednesday, 11 May 2022

VIJANA 50 WAKAMATWA KWA TUHUMA ZA UHALIFU MWANZA, DC MASALLA ATOA RAI KWA WAZAZI



Na Samir Salum, Lango la Habari-Mwanza

Jeshi la Polisi Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza limewakamata Vijana 50 wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu ikiwemo uporaji, kuvunja nyumba na kujeruhi.

Hayo yamethibitishwa leo Jumatano Mei 11,2022  na Kamanda wa Polisi Wilaya ya Ilemela SSP Elisante Ulomi katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Nyasaka Ikiwa mara baada ya wananchi kulalamikia kukithiri kwa vikundi vya kihalifu.

Kamanda Ulomi amesema kuwa Jeshi la Polisi linaendelea kufanya operesheni maalum dhini ya vikundi vya kihalifu ambapo hadi vijana 50 wamekamatwa.

Amesema kuwa vijana hao ni wenye umri kati ya miaka 17 hadi 23 ambao wameunda makundi ya kihalifu yakiwemo G7, Selebobo, Sanitizer,Barakoa na Covid.

“tunaendelea na operesheni kubwa ya kukamata vijana wanaojihusisha na uhalifu,hadi sasa tumekamata vijana zaidi ya 50, hatutaacha kufatilia makundi hayo” amesema SSP Ulomi

Ameongeza kuwa wapo wanaomiliki vikundi vya kihalifu wakiwemo baadhi ya viongozi wa Serikali ambapo amehidi kuchukua hatua dhidi yao.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masalla ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa kwa Jeshi la polisi juu ya uwepo wa vijana wanaofanya vitendo vya kihalifu na wahalifu.

“hao vijana wanafahamika,wakionekana tunaomba wananchi watoe taarifa kwa vyombo vya ulinzi na usalama ili tuweze kukomesha vitendo hivyo”amesisitiza DC Masalla

Aidha amewaasa wazazi kuwalea watoto wao katika maadili mema ili kuwaepusha watoto wao kujihusisha na vitendo vya kihalifu pamoja na viongozi wa dini kukemea vitendo hivyo.


Mwisho
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages