Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Mwanaidi Ally Khamis, akikabidhi zawadi za Eid El Fitr, kwa wazee wa Makazi ya Wazee waliopo katika kituo cha Nunge jiji Dar es Salaam.Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Mwanaidi Ally Khamis, akiwa kwenye picha ya Pamoja na Wazee waliopo kwenye Makazi ya Wazee yaliopo Nunge Kigamboni, Dar es Salaam.Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Mwanaidi Ally Khamis, akiongeaa mara baada yakukabidhi zawadi za Eid El Fitr, kwenye Makazi ya Wazee Nunge yaliyopo mkoani Dar es Salaam eneo la Kigamboni.Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Fatma Almas Nyangasa akitoa ombi maalum kwa watanzania na wadau mbali mbali kuendelea kujitokeza kwa ajili yakufika kwenye kambi za wazee na kuwajulia hali.Afisa Mfawidhi wa Makazi ya Wazee Nunge Jaqline Kanyemezi, akitoa taarifa ya Makazi ya hayo, wakati Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Mwanaidi Ally Khamis, alipofika kwenye kituo kwaajili ya sherehe za Eid El Fitr. Moja ya Nyumba ya Makazi ya Wazee, iliyopo Nunge mkoani Dar es Salaa, wilayani Kigamboni, ambayo Makazi hayo yamefanyiwa ukarabati, na hivi ndivyo muonekano wa Nyumba hizo kwa sasa.
************
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ally Khamis amesema kuelekea Sherehe za Eid El fitr, Wizara itahakikisha kundi la Wazee linasherekea sikukuu hiyo kwa furaha kama ilivyo kwa makundi mengine.
Naibu Waziri Mwanaidi amebainisha hayo akiwa katika Makazi ya Wazee Wasiojiweza Nunge, Kigamboni Mkoani Dar es Salaam alikokabidhi zawadi
ya Eid el Fitr.
“ Nimekuja hapa kuwaletea wazee wetu swadaka itakayowawezesha kusherekea kama watu wengine huko Duniani watakavyokuwa wanaserekea, Rais wetu (Mhe. Samia Suluhu Hassan) mara kwa mara amekuwa akisisitiza juu ya umuhimu wa kuwaenzi wazee hawa. Wakati wa ujana wao walitumia nguvu zao kulijenga taifa hili, sasa kwakuwa wao wamezeeka ni wakati wetu kuhakikisha tunawallinda na wanapata mahitaji yao ya Msingi” alisema Mwanaidi.
Naibu Waziri Mwanaidi alisema kwa sasa Wizara inaendelea kuyahudumia makambi yote 14 yaliopo chini ya Wizara kwa kuhakikisha mahitaji ya msingi kwa ajili ya wazee yanapatikana na kama kuna makazi ambayo yanachangamoto kinachofanyika ni kutatua changamoto hizo.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Fatma Nyangasa amewataka wadau mbalimbali watambue kuwa jukumu la kuwatunza wazee sio la Serikali peke yake bali pia wadau na mtu mmoja mmoja kwa nafasi yake kwa kuwa kufanya hivyo kunaongeza thawabu mbele ya mwenyezi Mungu.
“Wazee hawa wanaolelewa hapa Kigamboni na wengine kwenye Makazi mengine, niwombe watanzania wenzangu unapopata fursa tuwatembee na kuongea nao, lakini ukiwa na chochote basi ukiwapa itawasadia kwa namna moja au nyingine” amesema Nyangasa.
Awali akitoa taarifa ya Makazi hayo, Afisa Mfawidhi wa Makao hayo, Jaqline Kanyemezi ameishukuru Wizara kwa kuendelea kutoa fedha za uendeshaji wa Makazi hayo na kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza.
Kwa upande wao, wazee wanaoishi kwenye makazi hayo wameishukuru Serikali kwakuwakumbuka na kuja kuwajulia hali mara kwa mara.
MWISHO