Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) imeagiza kusitishwa kwa wimbo wa Diamond Platnumz Ft. Zuchu - Mtasubiri Sana, kutokana na kipande kinachomuonesha Zuchu akiimba kwaya kanisani na baadaye akaacha baada ya kupigiwa simu.
Mamlaka hiyo imesema kipande hicho kimeibua ukakasi na hisia za dharau juu ya dini/madhehebu fulani.