Kupitia ukurasa wake wa Twitter TCRA imesema: “Tumeona malalamiko kutoka kwa wadau mtandaoni kuwa watoa huduma wa mitandao ya simu wamebadilisha vifurushi kimyakimya, endapo kuna mtumiaji amenunua kifurushi, halafu akapata tofauti na kile alicholipia, awasiliane nasi.
“Mamlaka inafuatilia suala hili kwa watoa huduma ili kuweza kubaini ukweli.”
Watumiaji wa huduma hizo wameeleza kuwa kilichofanyika ni kwa fedha ileile unapata MB chache tofauti na ilivyokuwa awali, mfano unanunua kifurushi cha Tsh 2000 ulikuwa unapata GB 1, sasa hivi ukinunua kwa gharama ileile unapata MB 900 Aau MB 800.